Post Header
Programu ya Archive of Our Own – AO3 (Shirika la Maktaba Yetu) katika, yaani app, katika simu aina za Android ilitolewa katika Google Play. App ilioendelezwa si rasmi na imeleta tata kidogo.
"Mumefikiri kuendeleza programu ya simi rununu?" ni swali tunaloulizwa maa mengi. Tungependa kufanya hivi sana. Shida ni, app hizi lazime zitengenezwe tofauti kulingana na aina za simu rununu, kwa mfano, Android, iOS na Windows Mobile -- ambazo zinatumika mara mengi, bila hata kufikiri aina zingine.
Kabla tuanze hata kufikiri kuitengeneza app hio, kwanza ni sharti tuendeleze API ya umma. Mwendelezo huu uko katika mipango yetu ya baadaye, lakini si wakati karibu. Baada ya hayo, tungelazaimishwa kuiunda kwa njia inayoweza kutumika kwa simu rununu na pia kwa simu aina ya tablet. Ni mpango usiolekezwa kwa urahsi, una machangamano mengi na unahitaji watu waliojitolea kwa dhati, na wenye ustadi. Ingawa tungependa sana kuendelea na mradi wenyewe, kwa wakati huu hatuna wakati wala rasilimani kufanya hivyo.
Coders ambao waliunda AO3 walifanya hivyo kujitolea kihiari, kutumia wakati wao. Rasilimali yetu sasa hivi inatumika kuendeleza AO3 na kutatua shida zozote.
Kuendeleza mradi wa programu wa simu rununu, timu yetu italazimishwa kupuuza kazi zao za kawaida. Hatuna wafanyikazi wa kuendeleza miradi hii mbili sawia.
Na sio tu undelezaji wa mwanzo ambao unahitaji rasilimali yetu yote. Kudumisha app ni kazi ngumu, lazima itengenezwe upya ambapo tafsiri mpya wa simu rununu unatolewa. Pia, ni lazima app iboreshwe ambapo AO3 unaendeleza mambo mapya.
Ziada ya hayo, app inahitaji udumishi ambao hauwezi kuendelezwa na michango tunayopata.
Coding na kutahini rasilimali si matata tu tunayokumbwa nayo. Tungehitaji pia usaidizi kutoka timu zinazofuata:
- Wanaxhama wa timu ya Usaidizi wangefunzwa kutatua shida za kiteknolojia zinazokumba app yenyewe,
- Timu ya uandikaji wa hati, yaani documentation watalazimishwa kuunda na kufanya upya hati za app na
- Timu ya Utafsiri italazimishwa kushinda kutafsiri nyaraka ili wenye hawaongei lugha ya Kiingereza wataweza kuituimia app.
Kuendelea na miradi hii si halisi, inazidisha rasilimali yetu na pia itazuia wafanyikazi wetu kuendelea na kazi zao za kawaida.
Lengo letu ni kuendeleza AO3 na kuhaikisha inaweza kutumika na watu wote. Jinsi tutatumiza lengo letu ni kutia mkazo nguvu zetu zote kwa kujenga tafsiri la AO3 ambayo inafanya kazi kwa simu na tarakilishi za aina zote, licha ya umbo au ukubwa. Tutaendelea kusisitiza hii kama lengo letu kuu.
Inamaanisha, uundaji wa app hauwezekana wakati huu, pengine baadaye.
Kuwa mwangalifu kuhusu usalama, ambapo app au tovuti isiyohusika na AO3 inakuuliza kuhusu utondoti kama nenosiri lako.
Tahadhari na kama unafikiri akaunti yako imetiwa hatarini, usisite kubadilisha nenosiri lako wakati wowote.
Nyaraka hii ilitafsiriwa na watafsiri wa OTW. Watafsiri hawa ni wa kujitolea kwa hiari. Kujua mengine kuhusu kazi yetu, tafadhali tazama Ukurasa wa utafsiri katika transformativeworks.org.
